Straika Simba Atimkia Uturuki-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Straika Simba Atimkia Uturuki-Michezoni leo

STRAIKA na kinara wa mabao wa Simba Queens, Opah Clement, usiku Machi 4 alipaa kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kujiunga na timu ya Yikatel Kayseri inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini humo.

 

Meneja wa kikosi hicho, Selemani Makanya, amelithibitishia Championi Jumamosi, juu ya straika huyo kuondoka kikosini humo baada ya Waturuki hao kutuma barua ya kumhitaji.

 

“Ni kweli Yikatel Kayseri iliwasilisha barua ya kuhitaji huduma ya Opah Clement na ameelekea nchini uturuki kujiunga nao.”

 

Opah ndiye kinara wa mabao ndani ya Simba Queens kwa msimu huu akifunga mabao 19, pia akiiacha timu hiyo ikiongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 33.

The post Straika Simba Atimkia Uturuki appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz