Siri 2 za msako wa ubingwa Yanga SC zafichuka-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Siri 2 za msako wa ubingwa Yanga SC zafichuka-Michezoni leo

KAMA unafikiri Yanga wana mpango wa kushuka kutoka nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu, basi umejidanganya na ndio kwanza wameweka wazi kuwa wanahitaji kupata matokeo katika michezo yote ili waweze kutwaa ubingwa msimu huu, hasa kwa kupata ushindi dhidi ya KMC katika mchezo unaofuata.

Lakini Injinia Hersi Said amefichua siri mbili ambazo wanazitumia kusaka ubingwa msimu huu waliodhamiria ni lazima wabebe taji la Ligi Kuu Bara kwa namna yoyote ile.

Hersi ametaja siri ya kwanza kuwa ni kuhangaika na mchezo unaofuata, yaani wanachowaza inakuwa ni mchezo unaofuata tu. Hesabu za mchezo mmoja baada ya mwingine.

Pili, wamezungumza na wachezaji wao na kuwaambia wauchukulie kila mchezo kama fainali. Yanga ambao ndio vinara wa ligi kuu kwa sasa, watacheza dhidi ya KMC katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Machi 19 wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa kwanza katika mzunguko wa awali kwa mabao 2-0.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Injinia Hersi Said, alisema kuwa malengo yao kwa sasa ni kuhakikisha wanapata alama katika kila mchezo unaofuata kutokana na mzunguko wa pili kuwa mgumu, jambo ambalo tayari wameshazungumza na wachezaji kwenye michezo hii ya mzunguko wa pili kuhakikisha wanaondoka na ushindi hasa katika mchezo unaofuata dhidi ya KMC.

“Kwa sasa hatufikirii kuwa tutacheza michezo mingapi iliyobaki na kuanza kuhesabu mechi ya ubingwa, ambacho tumewaambia wachezaji ni kwamba kila mchezo ni kama fainali kwetu katika huu mzunguko wa pili, hivyo ambacho tunatakiwa kufanya ni kushinda katika mchezo ambao upo karibu yetu.

“Mfano kwa sasa tunafikiria kuhusu mchezo wetu unaofuata dhidi ya KMC na wala hakuna kingine ambacho tunawaza, tunahitaji kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ili tuendelee kukaa kileleni,” alisema kiongozi huyo.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Siri 2 za msako wa ubingwa Yanga SC zafichuka appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz