Simba Yawaingiza Chaka ASEC Mimosas-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Yawaingiza Chaka ASEC Mimosas-Michezoni leo

WAPINZANI wa Simba, ASEC Mimosas ya nchini Ivory Coast, wajiandae kukutana na sapraizi mara watakapokutana katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Timu hizo ambazo zipo Kundi D, zinatarajiwa kuvaana Jumapili hii katika mchezo wa tano hatua ya makundi kunako michuano hiyo utakaopigwa nchini Benin.

 

Simba inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 7, ASEC pointi 6 sawa na RS Berkane, huku US Gendarmerie ikiwa mkiani ikikusanya pointi 4.

 

Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, juzi aliomba mchezo wa kirafiki dhidi ya Akademi ya Cambiasso uliochezwa Simba Mo Arena, Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa kirafiki, Pablo aliwatumia zaidi wachezaji ambao hakuwatumia mechi dhidi ya RS Berkane, Jumapili iliyopita ambapo Simba ilishinda 1-0, Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Kikosi kilichotumika katika mchezo huo wa kirafiki kilikuwa hivi; Beno Kakolanya, Israel Patrick, Gadiel Michael, Pascal Wawa, Kenedy Juma, Erasto Nyoni, Bernard Morrison, Taddeo Lwanga, Chris Mugalu, Clatous Chama na Jimmyson Mwanuke.

 

Pablo alimtumia Lwanga raia wa Uganda kucheza dakika zote tisini, akimchezesha namba 8, huku namba 6 akicheza Nyoni ambaye alifunga bao la kusawazisha katika ushindi wa 2-1 walioupata Simba. Bao lingine likifungwa na Chama.

 

Kutokana na Lwanga kucheza mechi hiyo kwa dakika zote tisini na kuonekana kuwa fiti akirejea uwanjani akitoka kuuguza majeraha ya goti, huenda mechi dhidi ya ASEC akaanza tofauti na alivyoingia dakika ya 80 dhidi ya RS Berkane.

 

Pablo alisema: “Kila mchezaji hapa ana nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza, zaidi ninafurahia kuona wachezaji wenye majeraha wakipona.

 

“Kupona kwa wachezaji hao kunanipa wigo wa kuchagua mchezaji yupi nimtumie katika mchezo husika utakaokuwa mbele yetu kwa lengo la kupata matokeo mazuri.”

 

Kesho Ijumaa alfajiri, jeshi kamili la Simba linatarajiwa kusafiri kutoka Dar kuelekea Benin kucheza dhidi ya ASEC.

WILBERT MOLANDI,
Dar es Salaam

The post Simba Yawaingiza Chaka ASEC Mimosas appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz