PSG Yapigwa 3-1 na Real Madrid Yatupwa Nje UEFA-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

PSG Yapigwa 3-1 na Real Madrid Yatupwa Nje UEFA-Michezoni leo

Mauricio Pochettino yupo kwenye presha ya kufutwa kazi ndani ya kikosi cha PSG baada ya timu hiyo kutolewa katika mbio za kuwania ubingwa wa UEFA Champions League na Real Madrid hapo jana.

PSG wametolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya jana kukubali kichapo cha mabao 3-1 katika mchezo wa mkondo wa pili uliochezwa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Karim Benzema aliondoka na mpira baada ya kuweka kambani magoli matatu (hat trick), huku bao la PSG likifungwa na Kylian Mbappe.

Inaelezwa kuwa Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ameonesha kutopendezwa na matokeo hayo jambo linaloonesha kwamba maisha ya Pochettino ndani ya klabu hiyo ya jijini Paris, Ufaransa yanakaribia kufika ukingoni.

WAUMINI WA MFALME ZUMARIDI WALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI KUSIKILIZA DHAMANA YAO..

The post PSG Yapigwa 3-1 na Real Madrid Yatupwa Nje UEFA appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz