Pablo: Tutacheza Kibingwa Kwa Mkapa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pablo: Tutacheza Kibingwa Kwa Mkapa-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya RS Berkane, benchi la ufundi la timu hiyo linafanya maandalizi makubwa kuhakikisha si tu kwamba kikosi chao kinaibuka na ushindi dhidi ya Berkane, lakini pia kinatoa burudani ya kibingwa.

 

Simba wanatarajia kuvaana na Berkane keshokutwa Jumapili katika mchezo wao wa nne wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya pointi nne katika michezo yao mitatu ya awali wakishinda mchezo mmoja, sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja.

 

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kwenye kundi lao D, wanakamata nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zao nne, huku RS Berkane wao wakiwa ndio vinara wa msimamo na pointi zao sita walizokusanya katika michezo mitatu.

Akizungumza na Championi Ijumaa, kocha Pablo alisema: “Tunatarajia mchezo mgumu dhidi ya Berkane Jumapili, huu ni mchezo wa maamuzi mchezo ambao timu itakayoshinda itakuwa moja kwa moja inaongoza msimamo wa kundi hili, hivyo ni mchezo muhimu sana kwa kila mmoja.

 

“Lakini jambo zuri kwetu ni kuwa kwa sasa tupo katika kiwango kizuri na tutakuwa kwenye uwanja wa nyumbani, hivyo hatutacheza tu kwa ajili ya kutafuta matokeo lakini ni lazima tuonyeshe kiwango bora kama ambacho tulionyesha katika michezo yetu miwili iliyopita ya ligi kuu.”

STORI NA JOEL THOMAS | CHAMPIONI IJUMAA

The post Pablo: Tutacheza Kibingwa Kwa Mkapa appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz