Pablo: Hatutoki Kileleni Shirikisho-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pablo: Hatutoki Kileleni Shirikisho-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Mhispania, Pablo Franco, amesema malengo yake ni kuhakikisha timu hiyo haishuki kileleni na kumaliza vinara wa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika, ili wajihakikishie nafasi ya kufanya vizuri zaidi hatua ya robo fainali.

 

Simba ikiwa inaongoza Kundi D ikikusanya alama saba, ikimaliza kinara kuna uwezekano mkubwa wa kutokutana na timu vigogo kama Pyramids, Orlando Pirates na Al Masry, zinazoongoza makundi yao.

 

Akizungumzia ishu hiyo, Pablo alifunguka kwamba: “Malengo yetu kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu ni kucheza angalau nusu fainali.

 

“Katika kufanikisha hilo, tunapaswa kufanya kazi kubwa michezo miwili ya mwisho ili kupata matokeo yatakayotuvusha.

“Tunataka kumaliza vinara wa kundi hili, ambapo hiyo itatusaidia kwa kiasi kikubwa kuwa na bahati ya kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani hatua ya robo fainali.”

 

Simba itashuka dimbani Machi 20 mwaka huu ugenini kuwavaa ASEC Mimosas, kabla ya kumalizana na US Gendarmerie, Aprili 3, mwaka huu, Dimba la Mkapa, Dar.

The post Pablo: Hatutoki Kileleni Shirikisho appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz