Pablo aweka mkakati mzito robo fainali Caf-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pablo aweka mkakati mzito robo fainali Caf-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameweka wazi kuwa hesabu zao ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika michezo yao iliyosalia ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ili kumaliza kileleni mwa msimamo wa Kundi D, hali itakayowafanya wapate ahueni ya kukutana na ‘kibonde’ katika michezo ya robo fainali.

Pablo anataka kikosi chake kimalize kinara wa Kundi D, kwa kuwa kanuni za mashindano zinampa nafasi ya kinara wa kundi kukutana na timu iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi jingine, ambayo kwa kawaida inakuwa kibonde kulinganisha na zile zilizomaliza vinara kwenye makundi yao.

Simba jana Jumapili walikuwa na kibarua cha mchezo wao wa nne wa hatua ya makundi dhidi ya RS Berkane ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, ambapo wamesaliwa na michezo miwili tu kutamatisha hatua hiyo, ule wa ugenini dhidi ya ASEC Mimosas na wa nyumbani dhidi ya USGN.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha, Pablo alisema: “Malengo yetu kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho msimu huu ni kuhakikisha tunacheza angalau nusu fainali, na katika kufanikisha hilo ni wazi tunapaswa kufanya kazi kubwa katika michezo yetu ya mwisho ili kuhakikisha tunapata matokeo.

“Tunataka kumaliza kama vinara wa kundi hili, ambapo hiyo itatusaidia kwa kiasi kikubwa kukutana na mpinzani ambaye atakuwa sio kiongozi wa kundi jingine katika hatua ya mtoano jambo litakalotupa ahueni zaidi.”

JOEL THOMAS, DAR ES SALAAM

The post Pablo aweka mkakati mzito robo fainali Caf appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz