Pablo Amuondoa Dilunga Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pablo Amuondoa Dilunga Simba-Michezoni leo

KUFUATIA majeraha ya muda mrefu ambayo ameyapata kiungo wa Simba, Hassan Dilunga, ambayo yanaweza kumuweka nje ya uwanja mpaka mwishoni mwa msimu huu, Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amefikia uamuzi wa kumuondoa nyota huyo kwenye mipango yake.

 

Dilunga alipata majeraha ya goti Februari 9, mwaka huu akiwa mazoezini na kikosi cha Simba kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

 

Nyota huyo ndiye mchezaji pekee wa Simba ambaye ni majeruhi kwa sasa, ambapo kutokana na jeraha hilo amekosekana kwenye michezo sita ya Simba kwenye michuano yote.

 

Simba jana walitarajiwa kurejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USGN, utakaopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha Pablo alisema: “Kuhusiana na Dilunga mwanzo hatukudhani angekuwa na jeraha kubwa ambalo lingemuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

“Lakini kwa bahati mbaya tunaweza kumkosa labda mpaka mwishoni mwa msimu, hivyo tunalazimika kumuondoa kwenye mipango yetu kwa sasa mpaka pale taarifa za timu yetu ya madaktari itakapoonyesha kuwa yupo tayari kujiunga na timu.”

STORI: JOEL THOMAS

The post Pablo Amuondoa Dilunga Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz