Morrison amchimba Mkwara Ibenge “Kwa Mkapa Hutoki”-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Morrison amchimba Mkwara Ibenge “Kwa Mkapa Hutoki”-Michezoni leo

Kiungo mshambuliaji wa Simba Sc, Bernard Morrison ‘BM3’ amemkaribisha Kocha wake wa zamani, Florent Ibenge nchini Tanzania huku akimtisha kuwa katika mchezo wao na Simba, hawatatoka salama katika Dimba la Mkapa.

Ibenge ambaye ni Kocha Mkuu wa RS Berkane ya Morocco aewasili Tanzania na timu yajke hiyo jana Alhamisi, Machi 10, 2022 kwa ajili ya mchezo wa raundi ya nne hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaopigwa Jumapili Machi 13.

Kupitia Ukurasa wake wa Isntagram, Morrison ameandika; “Whenever I see you, it reminds me of the day you brought me from Ghana to Congo DR and told me that you will help me grow The rest is history the only sad thing is that at Mkapa Stadium we forget what you’ve done nobody survives here.

Welcome to Dar Es Salaam Father

Kila nikikuona inanikumbusha siku ambayo ulinitoa kutoka Ghana hadi Congo DR na kuniambia utanisaidia kukua Mengine ni historia cha kusikitisha tu ni pale kwa Mkapa Stadium tunasahau ulichofanya. Hakuna anayepona hapa.

Karibu Dar Es Salaam Baba.”

Katika mchezo wa kwanza kati ya Simba na Berkane uliopigwa Morocco, Simba aliambulia kichapo cha bao 2-0, hivyo ana kila sababu ya kuhakikisha anautumia vizuri uwanja wa nyumbani kuhakikisha anapata alama tatu muhimu.

Ikumbukwe kuwa, Morrison aliwahi kuitumikia AS Vita Club ya Congo DR msimu wa mwaka 2016, ambayo Kocha wake mkuu alikuwa Ibenge.

The post Morrison amchimba Mkwara Ibenge “Kwa Mkapa Hutoki” appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz