Lwanga Afungua Mdomo Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Lwanga Afungua Mdomo Simba-Michezoni leo

BAADA ya kukaa nje kwa muda mrefu bila kucheza ndani ya Simba, kiungo wa timu hiyo, Taddeo Lwanga, amefungua mdomo kwa mara ya kwanza akidai sasa yupo fiti.

 

Lwanga alisema alikuwa na muda mrefu wa kuuguza majeraha yake, hivyo kwa sasa kila kitu kipo sawa na muda wowote ataingia uwanjani kuitumikia Simba.

 

Akizungumzia maendeleo yake akiwa Morocco alikokwenda na wenzake kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane, Lwanga alisema:

 

“Nilipata majeraha mwezi Oktoba, mwaka jana katika mchezo dhidi Jwaneng Galaxy.

 

“Jeraha lilikuwa kubwa, namshukuru Mungu nimepona na nipo tayari kurudi uwanjani na mashabiki watarajie kuniona hivi karibuni hasa kwenye raundi ya pili.”

 

Urejeo wa Lwanga ndani ya kikosi cha Simba, unazidi kuongeza uimara wa timu hiyo hasa kwenye safu ya kiungo. Simba sasa watakuwa na machaguo ya nani wa kuanza kati ya Jonas Mkude au Lwanga kucheza kama namba sita kwenye mzunguko wa kwanza.

Stori:Issa Liponda

The post Lwanga Afungua Mdomo Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz