Kisinda Aionya Simba Kwa Mkapa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kisinda Aionya Simba Kwa Mkapa-Michezoni leo

WINGA wa RS Berkane ya Morocco, Tuisila Kisinda amesema kuwa kucheza na Simba wakiwa ugenini katika Uwanja wa Mkapa, Dar sio sababu ya wao kupoteza mchezo huo.

 

Timu hizo zitakutana tena Machi 13, katika uwanja huo baada ya hivi karibuni kuvaana nchini Morocco na Simba kupokea kichapo cha mabao 2-0 ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi.

 

Kisinda ambaye aliichezea Yanga msimu uliopita ameliambia Championi Jumamosi, kuwa kucheza uwanjani hapo hakuwafanyi wao kupoteza mechi hiyo kwani malengo yao ni kupata matokeo mazuri katika michezo yao yote inayofuata ili wafike mbali.

 

“Malengo yetu safari hii ni kuweza kufika mbali katika michuano hii, hivyo tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunafanya vizuri katika kila mchezo uliosalia ili tuweze kutimiza malengo yetu.

 

“Sisi kucheza katika Uwanja wa Mkapa siamini basi itakuwa asilimia zote kwamba Simba watashinda mchezo huo, tunahitaji kupata matokeo mazuri tukiwa kwao japo wamekuwa na historia nzuri wakiwa katika uwanja wao,” alisema winga huyo.

 

The post Kisinda Aionya Simba Kwa Mkapa appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz