Chico Akabidhiwa Beki Mbishi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Chico Akabidhiwa Beki Mbishi-Michezoni leo

DAKTARI wa Viungo wa Yanga raia wa Tunisia, Yussef Ammar, amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mkongomani, Chico Ushindi ataanza kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC anayocheza beki mbishi, Hassan Kessy, hivyo wawili hao kuna uwezekano mkubwa kukutana.

 

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, utapigwa Machi 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Chico amekosa michezo minne hadi sasa kutokana na maumivu ya misuli aliyoyapata akiwa mazoezini, siku moja kabla ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Biashara United, Februari, mwaka huu.

 

Michezo aliyoikosa Chico ni dhidi ya Biashara United, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na anatarajiwa kuukosa mchezo wa Jumapili hii dhidi ya Geita Gold utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ammar alisema Chico amepona maumivu hayo na wiki ijayo ataanza mazoezi magumu baada ya kumaliza program binafsi.

 

“Chico amepata nafuu ya maumivu yake, hivi sasa yupo katika program ya mazoezi maalum ya binafsi chini ya usimamizi wangu ambayo ataimaliza Ijumaa hii.

 

“Baada ya hapo ataanza mazoezi magumu ya pamoja na wenzake ya uwanjani katika kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya KMC tutakaoucheza Uwanja wa Mkapa,” alisema Ammar.

STORI NA WILBERT MOLANDI

The post Chico Akabidhiwa Beki Mbishi appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz