Adebayor Awaandalia Sapraizi Simba Uwanja wa Mkapa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Adebayor Awaandalia Sapraizi Simba Uwanja wa Mkapa-Michezoni leo

Mshambuliaji wa US Gendarmerie, Victorien Adebayor.

KIUNGO mshambuliaji wa US Gendarmerie, Victorien Adebayor, ameweka wazi kuwa atahakikisha anapambana kwa nguvu ili kuisaidia timu yake kupata ushindi dhidi ya Simba,Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mchezo huo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho utapigwa Jumapili ya Aprili 3, unatarajia kuwa mkali kwani kila timu ina nafasi ya kwenda robo fainali ikiwa itashinda mchezo huo, wageni wanatarajia kutua nchini kesho Alhamisi.

 

Licha ya hivyo, Adebayor ambaye amefunga mabao matatu kwenye michuano hiyo anahusishwa kutakiwa na Simba na hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Try Again aliweka wazi kuwa wangependa kumsajili nyota huyo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Adebayor alisema kuwa. “Licha ya mchezo huu na Simba kuwa muhimu sana kwetu na kwao ila nitakuwa na furaha sana kuwaona mashabiki wa Simba na kuweza kucheza nao nyumbani.
“Kwa upande wangu maandalizi ya mchezo huo yapo vizuri na sina presha yoyote kuelekea mchezo huo na nitajitahidi kufanya vizuri ili kuisaidia timu yangu.”

The post Adebayor Awaandalia Sapraizi Simba Uwanja wa Mkapa appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz