Abramovic Awachanganya Mashabiki-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Abramovic Awachanganya Mashabiki-Michezoni leo

BILIONEA Roman Abramovich ametoa ujumbe unaoonyesha kuwa amejiuzulu kuimiliki Chelsea lakini bado ujumbe huo hauko wazi sana.

Hiyo ni baada ya Mrusi huyo kuonekana kuwa na ukaribu na Rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye majeshi yake yameleta vita kwa kuivamia Ukraine.

Mmiliki huyo aliyeinunua Chelsea Julai 2003, alitoa ujumbe kama wa kujiuzulu kwenye tovuti ya klabu hiyo juzi usiku.

Abramovich aliandika: “Wakati wa karibu miaka 20 ya umiliki wangu wa Chelsea FC, daima nimekuwa nikitathmini wajibu wangu kama kiongozi wa klabu, ambaye kazi yake ni kuhakikisha tuna mafanikio, pamoja na kujenga kwa ajili ya siku zijazo, huku pia tukiwa na msaada kwenye jamii.

“Daima nimekuwa nikifanya maamuzi kwa faida ya klabu. Bado ninasimamia misingi hii.

“Ndiyo maana leo ninatoa kwa wengine umiliki wa Taasisi ya Misaada ya Chelsea na uangalizi wa Chelsea FC. Ninaamini (watakaochukua nafasi) kwa sasa wapo katika nafasi nzuri ya kuangalia ubora wa klabu, wachezaji, wafanyakazi na mashabiki.”

Baada ya tamko hilo, mashabiki wa Chelsea wamechanganywa wakiwa hawajui kama ndio ameachia ngazi moja kwa moja au la.

The post Abramovic Awachanganya Mashabiki appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz