Simba Yawatumia Wamorocco Kuwavuruga Berkane-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Yawatumia Wamorocco Kuwavuruga Berkane-Michezoni leo

NI jino kwa jino huko Morocco. Katika kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa keshokutwa Jumapili dhidi ya RS Berkane, uongozi wa Simba umeamua kutumia uhusiano wao na maofisa wa Raja Casablanca ya Morocco kuhakikisha wanapata mbinu za kuwamaliza Berkane.

 

Simba inanufaika kutokana na kuwa na makubaliano ya ushirika na Klabu ya Raja Casablanca yaliyotokana na ziara ambayo aliifanya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez mwaka jana katika nchi za Morocco na Misri.

 

Akizungumzia mapokezi yao kutoka kwa uongozi wa Raja Casablanca ya Morocco baada ya kuwasili nchini humo, Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, alisema:

 

“Tunashukuru kwa kufanikiwa kufika salama hapa Morocco baada ya safari ndefu kutokea nchini Uturuki, ambapo tulikuwa na mapumziko ya muda mfupi baada ya kutokea nchini Niger.

 

“Jambo lililotufurahisha zaidi ni mapokezi mazuri ambayo tumeyapata kutoka kwa uongozi wa Klabu ya Raja Casablanca ya hapa ambao kwa kiasi kikubwa wameshirikiana na viongozi wetu waliotangulia hapa kuhakikisha tunafikia mahali salama na pia kupeana uzoefu juu ya wapinzani wetu na kuhakikisha tunafanya vizuri.” Simba ikiwa Morocco inatumia pia basi kubwa la Raja Casablanca katika mishe zote nchini humo.

JOEL THOMAS, Dar

RUSSIA vs UKRAINE: CHANZO KAMILI CHA UGOMVI WAO NI HIKI, WALIANZA KAMA UTANI, SASA WANATIKISA DUNIA!

The post Simba Yawatumia Wamorocco Kuwavuruga Berkane appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz