NI MISRI YA SALAH NA SENEGAL YA MANE FAINALI AFCON 2021-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

NI MISRI YA SALAH NA SENEGAL YA MANE FAINALI AFCON 2021-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

TIMU ya taifa ya Misri imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa penalti 3-1 kufuatia sare ya bila kufungana na wenyeji, Cameroon ndani ya dakika ya 120 usiku wa Alhamisi Uwanja wa Paul Biya Jijini Yaoundé.
Kipa wa klabu ya Zamalek, Mohamed Abou Gaba ‘Gabaski’ ndiye aliyeibuka shujaa wa Mafarao kwa kucheza penalti mbili za nyota wa Simba Wasiofungika, Harold Moukoudi na James Lea Siliki, wakati mkwaju wa zamani wa Tottenham Hotspur, Clinton N'Jie uliota mbaya.
Waliofunga penalti za Misri ni
Ahmed Mostafa Mohamed ‘Zizo’,  Mohamed Abdelmonem na  Mohanad Lasheen na sasa Mafarao watakutana na Senegal katika Fainali tamu ya AFCON 2021 Jumapili hapo hapo Paul Biya .
Kocha wa Mreno wa Misri, Carlos Queiroz alitolewa kwa kadi nyekundu na refa Mgambia, Bakary Papa Gassama baada ya kupingana na maamuzi kipindi cha pili.
Utakuwa usiku mzuri wa kuwashudia washambuliaji wawili nyota wa Liverpool, Mohamed Salah wa Misri na Sadio Mane wa Senegal wakiyapigania mataifa yao baina yao uwanjani.
Cameroon watajaribu kupoza machungu kwa kumenyana na Burkina Faso katika mechi y kuwania nafasi ya tatu, ambayo itachezwa Jumamosi.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz