Mtoto auawa na kuwekwa ndani ya sandarusi - EDUSPORTSTZ

Latest

Mtoto auawa na kuwekwa ndani ya sandarusiPENDO   Athumani  (3), mkazi wa kata ya Nyihogo Manispaa ya Kahama, amekutwa ameuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kufungwa katika mfuko wa sandarusi na  kutupwa nyuma ya nyumba aliyokuwa akiishi na mama yake mzazi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyihogo,  Idd   Mitimingi, alibainisha hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili  ofisini kwake kuhusiana na mauaji hayo ambayo yalitokea Februari 9,  mwaka huu.

Alisema mtoto huyo  aliokotwa akiwa amekufa siku moja baada ya kupotea na kwamba  mzazi wake alikuwa akiendelea kumtafuta.

Mitimingi alisema, awali alipatiwa taarifa za kupotea kwa mtoto huyo kabla ya kupatikana akiwa amefariki dunia na baada ya kukagua mwili huo ulionyesha dalili za kunyongwa.

“Mtoto bado mdogo na alikuwa bado anahitaji malezi ya baba na mama. Alipotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mujibu wa mama yake mzazi  lakini amepatikana akiwa amekufa tena kwa kufungwa kwenye sandurusi na kutupwa nyuma ya nyumba aliyokuwa akiishi,” alisema Mitimingi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paulo, alithibitisha kutokea mauaji hayo na kwamba mtoto huyo alinyongwa na watu wasiojulikana na kutupwa.

Alisema upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaini wahusika waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz