Mayele Amkosesha Usingizi Beki Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mayele Amkosesha Usingizi Beki Simba-Michezoni leo

BEKI wa kati wa Simba anayekipiga kwa mkopo Mtibwa Sugar, Ibrahim Ame, amesema mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani, Fiston Mayele ameshindikana huku akisisitiza amemkosesha usingizi.

 

Kauli ya beki huyo imekuja baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kumalizika kwa Yanga kuwafunga Mtibwa mabao 2-0 juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

 

Ame alisajiliwa na Simba msimu uliopita akitokea Coastal Union ya Tanga ambaye msimu huu alitolewa kwa mkopo Mtibwa pamoja na Said Ndemla na Jeremiah Kisubi.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ame alisema kuwa kabla ya mchezo huo, alipewa jukumu la kumkaba Mayele kwa lengo la kutofunga, lakini imeshindikana baada ya kumruhusu mshambuliaji huyo kufunga bao. Ame alisema kuwa bao hilo alilofunga Mayele, limemfanya akose furaha na amani huku akishindwa kupata usingizi.

 

Ame ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya bao hilo kutokana na maumivu, alionekana akiwa chini nje ya uwanja akisononeka. “Mayele ni mshambuliaji hatari na wa kuchungwa akiwa uwanjani kutokana na kiwango chake bora.

 

“Nakumbuka kabla ya mchezo wetu huo, nilipewa jukumu la kutembea na Mayele kila sehemu kwa lengo la kutofunga, lakini ikashindikana na kupata upenyo akafunga.

 

“Kiukweli nilifanya jitihada nyingi za kutosha za kuhakikisha Mayele hafungi lakini nimeshindwa, alitumia nafasi moja aliyoipata kufunga, kiukweli siku yangu imeharibika baada ya bao hilo, sitaweza kupata usingizi,” alisema Ame.

WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA, Dar

The post Mayele Amkosesha Usingizi Beki Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz