Yanga Yatumia Sh 50Mil Kuwapora Straika Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yatumia Sh 50Mil Kuwapora Straika Simba-Michezoni leo

IMEFAHAMIKA kuwa uongozi wa Yanga umetumia Sh 50Mil kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa Mbeya Kwanza, Chrispin Ngushi aliyekuwa akiwindwa pia na Simba na kumpa mkataba wa miaka mitatu.


Usajili wa Ngushi
mwenye mabao matatu akicheza michezo 11 ya Ligi Kuu Bara msimu huu, ni wa nne kwa Yanga
kusajiliwa kipindi hiki cha
usajili wa dirisha dogo uliofunguliwa Desemba 16, 2021.


Wachezaji wengine
waliosajiliwa na Yanga na kutambulishwa ni Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ kutoka Azam FC, Denis Nkane (Biashara United) na Aboutwalib Mshery (Mtibwa Sugar).


Kwa mujibu
wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mshambuliaji huyo amesajiliwa kwa dau hilo baada ya pande
zote mbili za
Yanga na Mbeya Kwanza kufikia muafaka mzuri.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, katika makubaliano hayo, ni lazima asaini mkataba wa miaka mitatu kutokana na umri wake mdogo aliokuwa nao utakaomfanya adumu muda mrefu katika soka.


Aliongeza kuwa, dau
hilo la usajili litakwenda sambamba na mshahara wa Sh 3Mil kwa kila mwezi kwa kipindi chote
atakachokuwepo
Yanga pamoja na kukaa katika apartment nzuri ya kisasa.


“Haikuwa M
kazi rahisi kufanikisha saini ya Ngushi kutoka Mbeya Kwanza kuja Yanga, kwani kulikuwepo na
vita kubwa kutoka
kwa wapinzani wetu (Simba) ambao walikuwa wakihitaji saini yake.

 

“Usajili wake tulifanikisha wiki moja iliyopita kabla ya jana (juzi) kumtambulisha rasmi kwa kuachia picha zake zikimuonesha akisaini mkataba na Yanga.

 

“Kama uongozi tulifkia  uamuzi wa kumpatia ada ya uhamisho ya Sh 50Mil pamoja na mshahara wa Sh 3Mil kwa kila mwezi sambamba na apartment ambazo tumekuwa tukiwapa wachezaji wetu wa kigeni na wale wanaotoka nje ya Dar,” alisema mtoa taarifa huyo.


Makamu Mwenyekiti
wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alipotafutwa kuzungumzia hilo, alisema: “Dau la usajili
ni siri kati ya uongozi
wa timu na mchezaji husika, hivyo sitaweza kuzungumzia hilo.”

STORI: WILBERT MOLANDI, DAR ES SALAAM

The post Yanga Yatumia Sh 50Mil Kuwapora Straika Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz