Yanga Princess Yapanga Kuvunja Rekodi Ya Simba Queens-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Princess Yapanga Kuvunja Rekodi Ya Simba Queens-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema ‘Morinyo’ ameweka wazi kuwa anataka kufuta uteja mbele ya Simba Queens kwa kushinda kwenye mechi yao ya dabi itakayopigwa leo Jumamosi katika Uwanja wa Mkapa, Dar.


Kocha huyo
alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano kati ya timu hizo na Waandishi wa Habari uliofanyika jana Ijumaa katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

 


Edna alisema:
“Sina matokeo mazuri au Yanga Princess haina matokeo mazuri mbele ya Simba, ila huu ni mchezo na matokeo ni baada ya dakika 90, tumejiandaa kushindana na kushinda.”

Kwa upande wake nahodha wa Yanga Princess, Fatuma Mwisendi, alisema: “Tutahakikisha tunapambana, tutaonyesha mchezo mzuri na wa kiungwana ukizingatia kuwakikosi chetu kina wachezaji wazoefu, wengi wao wameshacheza dabi tofautinchini kwao, kwa hiyo sidhani kama mchezo wa kesho (leo) utatuzuia sisi kupata ushindi.”


Nahodha wa
Simba, Violeth Nicholas, alisema:“Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo huu, muhimu ni kuboresha muendelezomzuri tulionao kwenye ligi na kushinda mechi zetu na kubakia nafasi ya kwanza kwenyemsimamo.”

The post Yanga Princess Yapanga Kuvunja Rekodi Ya Simba Queens appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz