Yacouba Aanza Tizi Yanga Kurejea Uwanjani-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yacouba Aanza Tizi Yanga Kurejea Uwanjani-Michezoni leo

NI habari njema kwa mashabiki wa Yanga baada ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Yacouba Songne raia wa Burkina Faso kuanza mazoezi mepesi, huku akitarajiwa kurejea rasmi uwanjani baada ya mwezi mmoja kama hakutakuwa na mabadiliko yoyote.


Yacouba alipata majeraha ya goti
kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Novemba 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na Yanga kushinda 3-1.


Baada ya kuumia, Novemba 10,
mwaka huu Yacouba alipelekwa nchini Tunisia kwa ajili ya matibabu akiongozana na Dokta wa Viungo wa Yanga, Youssef Mohamed, huku taarifa za awali kutoka kwa daktari zikieleza atakaa nje kwa muda wa zaidi ya miezi minne.


Akizungumza na Spoti Xtra, Dokta
Youssef, alisema: “Kila kitu kipo sawa, kuhusu hali ya Yacouba kwa sasa anaendelea vizuri.


“Ameanza mazoezi mepesi ya peke
yake ambapo tunatarajia baada ya mwezi mmoja ataanza rasmi mazoezi na timu.”

STORI NA LEEN ESSAU, SPOTI XTRA

The post Yacouba Aanza Tizi Yanga Kurejea Uwanjani appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz