Wiki Moja Baada ya Kujiuzulu, Mkwasa Arejea Tena Ruvu Shooting-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Wiki Moja Baada ya Kujiuzulu, Mkwasa Arejea Tena Ruvu Shooting-Michezoni leo

KLABU ya Ruvu Shooting imethibitisha kurejea kwa Kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa aliyekua ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo tangu juma lililopita.

 

Mkwasa alitangaza kujizulu nafasi yake klabuni hapo siku moja baada ya kikosi cha Ruvu Shooting kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC kwa kufungwa mabao 4-1.

 

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Klabu hiyo yenye Maskani yake Makuu mjini Mlandizi mkoani Pwani amesema, Kocha Mkwasa amerejea kwenye majukumu yake na tayari amefanya usajili wa wachezaji sita katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.

 

“Charles Boniface Mkwasa amerejea kwenye majukumu yake ndani ya kikosi cha Ruvu Shooting, na tayari tumeshakamilisha sajili za wachezaji sita ambao tayari wapo kambini.” amesema Masau Bwire.

 

Baada ya kutangaza kujiuzulu nafasi ya Kocha Mkuu, Mkwasa alitoa sababu za kufanya hivyo kwa kusema kilichomsukuma kuondoka Ruvu Shooting ni matokeo mabovu, tangu walipoanza msimu huu 2021/22.

The post Wiki Moja Baada ya Kujiuzulu, Mkwasa Arejea Tena Ruvu Shooting appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz