Wafungaji Wanaoongoza kwa Mabao Simba Sc Msimu Huu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Wafungaji Wanaoongoza kwa Mabao Simba Sc Msimu Huu-Michezoni leo

Licha ya klabu ya Simba Sc kuanza vibaya msimu huu wa NBC Premier League, mshambuliaji wa klabu hiyo Meddie Kagere ameendelea kuweka rekodi zake ngumu ndani ya kikosi hicho kwa kufunga magoli mengi msimu huu.

 

Klabu ya Simba Sc mpaka sasa wamecheza jumla ya michezo 12 ya NBC Premier League (kabla ya mchezo wa Kagera Sugar Vs Simba Sc), katika michezo hiyo Meddie Kagere amefunga jumla ya magoli manne na ndiye kinara wa magoli msimu huu ndani ya kikosi cha Simba Sc.

 

Nafasi ya pili ya ufungaji bora ndani ya klabu ya Simba Sc inashikiliwa na mshambuliaji mpya wa timi hiyo Kibu Denis ambaye amejiunga na klabu ya Simba Sc akitokea katika klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya. Kibu Denis yeye amefanikiwa kufunga jumla ya magoli matatu kwenye michezo 12 ya klabu Simba Sc msimu huu.

 

Wachezaji wengine kama vile Mzamiru Yassin, Kanoute, Sakho, Mohammed Hussein, Peter Banda na Rally Bwalya wamefunga goli moja moja msimu huu.

 

Takiwimu hizi siyo siyo mbaya sana kwa msimu huu licha ya kwamba hazina uwihano mzuri na takwimu za msimu uliopita ambapo Simba Sc walikua na uwezo mkubwa wa kufunga magoli mengi wakiwa na washambuliaji wao hatari Chris Mugalu, Meddie Kagere, na Bocco ambao msimu huu wamekua na kiwango kibovu kwa kushindwa kufunga magoli mengi.

 

Simba Sc wanaendelea kurudi kwenye mfumo wao haswa baada ya kurejea kwa Clatus Chota Chama ambaye ametoka katika klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco siku chache zilizopita. Chama ni moja ya viungo bora ndani ya ligi hii ambapo tayari ameweka rekodi nyingi nzuri akiwa na Simba Sc misimu kadhaa iliyopita.

 

Endapo kama Chama ataendelea kucheza kwa kiwango chake kikubwa ni wazi kwamba washambuliaji wa klabu ya Simba Sc watakua kwenye nafasi ya kufunga magoli msimu huu kutokana na ukweli kwamba kiungo huyu anaweza kutengeneza nafasi nyingi za magoli akiwa katika eneo la ushambuliaji.

The post Wafungaji Wanaoongoza kwa Mabao Simba Sc Msimu Huu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz