Simba Yaachana na Nyoni, Yashusha Jembe Jipya-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Yaachana na Nyoni, Yashusha Jembe Jipya-Michezoni leo

UNAAMBIWA Simba wamekuja na staili ya kata mti panda mti, hii ni baada ya kuchukua maamuzi ya kuachana na kiungo mshambuliaji wao Mmalawi, Duncan Nyoni na kumalizana na kiungo Mzambia, Samuel Sikaonga.


Nyoni aliungana na Simba mwanzoni
mwa msimu huu, kwa mkataba wa miaka mitatu, akitokea Silver Strikers ya Malawi, lakini ameshindwa kuonyesha kiwango bora ndani ya timu hiyo jambo linalodaiwa kuwapelekea mabosi wake kumfungashia virago.


Chanzo chetu kutoka Simba, kimeliambia
Championi Ijumaa, kwamba, baada ya uongozi wa Simba kujadiliana kwa kina matakwa ya ripoti ya Kocha Mkuu Pablo Franco, umelazimika kukatisha mkataba na Nyoni ili utoe nafasi kwa kiungo Samuel Sikaonga.


“Ripoti ya kocha Pablo imeleta mabadiliko
na maamuzi mazito sana ndani ya Bodi ya Wakurugenzi, hasa upande wa kamati ya usajili, ambapo umekata majina takriban matatu ya nyota wetu na kuachana nao rasmi akiwemo Nyoni.


“Kocha hajaridhishwa na uwezo wa
Nyoni, jambo ambalo ameipa kamati ya usajili kutafuta mbadala wake, ambapo wao wameamua kumng’oa rasmi na kuingiza jina la Sikaonga ambaye atahudumu moja kwa moja katika nafasi ya Taddeo Lwanga,” kilisema chanzo hicho.

 

Championi Ijumaa lilimtafuta Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Simba, Barbara Gonzalez, ambaye simu yake ilikuwa haipokelewi hadi tunakwenda mitamboni, lakini mmoja wa vigogo wa Simba, ambaye hakutaka kuwekwa wazi alilithibitishia gazeti hili kuwa kweli wameshaachana rasmi naNyoni.

The post Simba Yaachana na Nyoni, Yashusha Jembe Jipya appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz