Simba: Tunawavua Yanga Ubingwa Mapinduzi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba: Tunawavua Yanga Ubingwa Mapinduzi-Michezoni leo

KUELEKEA mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi kesho Jumanne, uongozi wa Simba umetamba kuwa kikosi chao kiko tayari kwa ajili ya mashindano hayo na malengo yao makubwa ni kuwavua ubingwa watani zao wa jadi Yanga.


Michuano ya Kombe la Mapinduzi
ilianza rasmi jana Jumapili kwa mchezo mmoja kati ya Namungo dhidi ya Meli 4 City. Kuelekea michuano hiyo Simba leo inatarajiwa kusafiri kwenda Zanzibar kwa ajili ya michuano hiyo, ambapo msimu uliopita walicheza hatua ya fainali.


Simba juzi Jumamosi katika Uwanja
wa Mkapa Dar es Salaam walikuwa wenyeji wa Azam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 2-1, ushindi ambao umeifanya Simba kufikisha pointi 24 katika michezo 10 waliyocheza mpaka sasa.


Akizungumza na Championi
Jumatatu, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema: “Tunajivunia mwenendo ambao kikosi chetu umekuwa nao kwa sasa, baada ya kumaliza mchezo wetu uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Azam mipango yote ni kuelekea michuano ya Kombe la Mapinduzi.


“Tutakwenda kwenye michuano
hii tukiwa na ari na mipango ya kuhakikisha tunaibuka mabingwa, lakini pia hii itakuwa sehemu ya kikosi chetu kupata mazoezi ya ziada kwa ajili ya kuongeza muunganiko wa timu
hususani kwa nyota wapya ambao
watajiunga na kikosi chetu kwenye dirisha hili la usajili.”

STORI: JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Simba: Tunawavua Yanga Ubingwa Mapinduzi appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz