Simba Sc Watwaa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2022-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Sc Watwaa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2022-Michezoni leo

Simba SC imeandika hitoria mpya baada ya kubeba Kombe la Mapinduzi kwa kuitandika Azam FC kwa goli 1-0 katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

 

Hapo awali Simba ilipata kuingia fainali kadhaa za Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC lakini walijikuta wakipoteza lakini hii leo Kocha Pablo Franco ameandika historia mpya.

 

Goli pekee la ushindi katika mchezo huo limefungwa kwa mkwaju wa Penati na mshambuliaji Meddie Kagere kunako dakika ya 55 ya mchezo baada ya makosa ya mlindo mlango wa Azam, Mathias Kigonya kumchezea madhambi Sakho.

 

Mchezo huo ulitawaliwa na ufundi na kasi ya hali ya juu mpaka zinakamilika dakika 90 ni Simba ndio waliofanikiwa kujinyakulia taji lao la kwanza msimu huu.

 

Katika mchezo wa Fainali kulikuwa na maauzi kadhaa yaliyofanywa na mwamuzi ambayo walio wengi wlikua na mashaka nayo.

The post Simba Sc Watwaa Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2022 appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz