Simba, Azam ni Tambo Tu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba, Azam ni Tambo Tu-Michezoni leo

IKIWA imebaki siku moja kukamilisha hesabu za mwaka 2021, Januari Mosi 2022 unatarajiwa kuchezwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba  dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, huku timu zote zikitamba kusepa na pointi tatu.

 

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco, ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo na pointi zake 21 kibindoni, inatarajia kuwa mwenyeji wa Azam FC iliyo nafasi ya saba na pointi 15.Akizungumza na Spoti
Xtra, Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba, alisema: “Mechi zetu zote ambazo tutacheza ipo wazi kwamba ni ngumu hasa ukizingatia kwamba ligi ya msimu huu ina ushindani mkubwa lakini kwa yote ambayo tunakutana nayo tunachohitaji ni pointi tatu, hivyo tunafanya maandalizi mazuri.”


Kwa upande wa Azam
FC, Ofisa Habari, Zakaria Thabit, alisema: “Mchezo ambao unatukutanisha na
Simba, Yanga na KMC hii
huwa inakuwa na utofauti, lakini tunajua namna ya kukabiliana na wapinzani
wetu tunachohitaji ni pointi
tatu.

LUNYAMADZO MLYUKA,DAR

The post Simba, Azam ni Tambo Tu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz