Shiboub Aanza Kazi Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Shiboub Aanza Kazi Simba-Michezoni leo

KIUNGO raia wa Sudan, Sharaf Eldin Shaiboub Ali Abdelrahman ametambulishwa rasmi ndani ya Kikosi cha Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Klabu ya Simba leo Jumatatu, Januari 3, 2021 mchana Visiwani Zanzibar.

Shiboub ambaye msimu wa mwaka 2019–2020 aliitumikia Simba kabla ya kuachana nao, amerejea tena na tayari ameshatua Visiwani Zanzibar kuungana na kikosi cha timu hiyo ambayo itashiriki Kombe la Mapinduzi.

 

Imeelezwa kuwa, mechi za Mapinduzi ndizo yatakuwa majaribio ya Shiboub na iwapo atamridhisha Kocha Pablo Franco Martin, basi Simba watamsajili kwa mara nyingine katika Dirisha Dogo la usajili ambalo tayari limeshafunguliwa.

Shiboub amethibitishwa uwepo wake ndani ya Simba pamoja na kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast Moukoro Cheik Tenana ambaye pia atashiriki michuano hiyo ya mapinduzi kama majaribio kabla ya kusajiliwa. Wachezaji hao tayari wameshaanza mazoezi ndani ya Simba kwa ajili ya kuanza michuano ya Mapinduzi.

The post Shiboub Aanza Kazi Simba appeared first on Global Publishers.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz