TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kutwaa taji la Super Cup ya Hispania baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Barcelona katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 usiku wa Jumatano Uwanja wa King Fahd International Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Mabao ya Real Madrid yamefungwa na Vinicius Junior dakika ya 25, Karim Benzema dakika ya 72 na Federico Valverde dakika ya 98, wakati ya Barcelona yamefungwa na Luuk de Jong dakika ya 41 Ansu Fati dakika ya 83.
No comments:
Post a Comment