Real Madrid Yaitungua Barcelona na Kutinga Fainali-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Real Madrid Yaitungua Barcelona na Kutinga Fainali-Michezoni leo

Real Madrid imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Supercopa baada ya kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya mahasimu wao wa FC Barcelona katika mchezo wa El Clasico uliopigwa katika ardhi ya Saudia.

 

Mabao ya Madrid yamefungwa na Vinicius Jr , Karim Benzema na Federico Valverde akipachika bao la ushindi dakika ya 98 katika muda wa dakika 30 za ziada baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa sare ya 2-2.

 

Barcelona walipata mabao yake kupitia kwa Luuk De Jong na Ansu Fati aliyefunga akitokea benchi.

 

Sasa Real Madrid wanamsubiri Mshindi kati ya Atletico Bilbao na Atletico Madrid watakaokutana katika nusu fainali nyingine ya mashindano hayo yanayopigwa huko Riyadh Saudi Arabia.

The post Real Madrid Yaitungua Barcelona na Kutinga Fainali appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz