Pablo Awaweka Kitimoto Bwalya, Morrison Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pablo Awaweka Kitimoto Bwalya, Morrison Simba-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco ameweka wazi kuwa haridhishwi na namna ambavyo mastaa wa kikosi hicho wamekuwa wakishindwa kutumia faida ya mipira iliyokufa hususan penalti na tayari amekaa na mastaa hao ili kusaka suluhisho la changamoto hiyo.


Simba juzi Jumamosi
waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa
kwenye Uwanja wa Mkapa,
Dar es Salaam ambapo licha ya ushindi huo staa wao, Rally Bwalya alikosa mkwaju wa penalti.


Hii inakuwa ni penalti ya
tatu kati ya nne ambayo Simba wamekosa katika michezo yao mfululizo ambapo Bwalya
amekosa penalti
mbili, Morrison moja sawa na Erasto Nyoni.


Akizungumza
na Championi Jumatatu, Kocha Pablo alisema: “Tunashukuru kwa ushindi ambao tuliupata katika
mchezo wetu
dhidi ya Azam, kwetu huu ulikuwa ushindi muhimu.

 

Lakini licha ya ushindi huo niweke wazi kuwa nimeshangazwa sana na namna ambavyo tumekuwa na wakati mgumu kutumia faida ya mipira iliyokufa hususan penalti.


“Ukiangalia vizuri utagundua
kuwa tumekosa penalti tatu kati ya nne mfululizo kwenye michezo yetu iliyopita kupitia kwa wachezaji tofauti kama Morrison, Bwalya na Nyoni.


Ni kweli kukosa
penalti ni sehemu ya mchezo lakini hii haitoi taswira nzuri kwangu kama kocha na tayari nimeanza kulifanyia kazi hilo.”

Stori: JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Pablo Awaweka Kitimoto Bwalya, Morrison Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz