Pablo Aukubali Mziki wa Shiboub-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pablo Aukubali Mziki wa Shiboub-Michezoni leo

TAYARI uongozi wa Simba chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’umefikia makubaliano ya kuachana na beki Muivory Coast, Pascal Wawa ili ampishe kiungo raia wa Sudan, Sharaf Eldin Shiboub ambaye kiwango chake kimeonekana kumvutia Kocha Mkuu, Pablo Franco raia wa Hispania.


Wawa alijiunga na
Simba Julai 1, 2018 akitokea Al Merreikh ya Sudan iliyomsajili kutoka Azam FC msimu
wa 2015/2016 mara
baada ya mkataba wake kumalizika.


Shiboub amerejea
Simba akiwa mchezaji huru, huku klabu hiyo ikisema amekuja kufanya majaribio katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.


Kumbuka aliwahi
kuichezea Simba msimu wa 2019/20, kisha akatimkia CS Constantine ya Algeria. Taarifa ambazo
imezipata
Spoti Xtra, zinasema kwamba, licha ya viongozi kuficha Shiboub yupo nchini kwa majaribio, lakini
ukweli tayari bodi yao
kupitia kamati ya usajili imeshamkata Wawa kwa siri.


Mtoa taraifa huyo
alisema kuwa Shiboub tayari amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa siri na rasmi
atatambulishwa kati
ya Desemba 9 na 10, mwaka huu.


Aliongeza kuwa,
amepewa mkataba huo mfupi wa mwaka mmoja kwa ajili ya benchi la ufundi la timu hiyo,
chini ya Kocha Pablo
kuangalia kiwango zaidi.


“Upo uwezekanao
mkubwa wa Shiboub kuongezewa mkataba mwingine wa mwaka mmoja na kufikisha miwili, lakini kamaakionesha kiwango bora.


“Hiyo ni baada ya
hivi karibuni mara kutua nchini kusaini mkataba wa mwaka mmoja wenye sharti la
kuongezewa mwingine
kama atalishawishi benchi la ufundi kwa kiwango bora.


“Na jina la Wawa
litaondolewa katika usajili huo wa dirisha dogo, hivyo muda wowote uongozi utatangaza kuachana
na beki huyo ambaye
hivi karibuni amepoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza,” alisema mtoa taarifa huyo.


Mwenyekiti wa
Simba, Murtaza Mangungu, alizungumzia usajili hivi karibuni kwa kusema kuwa: “Kila kitu kinachohusiana na usajili tumepanga kutangaza hivi karibuni, licha ya kupokea ripoti ya kocha ilitoa mapendekezo ya wachezaji wa kusajiliwa na kuachwa katika dirisha dogo.”

STORI: MUSA MATEJA NA WILBERT MOLAND

The post Pablo Aukubali Mziki wa Shiboub appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz