Pablo Aanza na Majembe Mapya Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pablo Aanza na Majembe Mapya Simba-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameonyesha kuwa ni kweli hataki masihara, kwani mapema tu ameweka wazi kuwa atakuwa na programu maalum na majembe mapya ya kikosi hicho ili kuhakikisha wanaingia katika mfumo wake na kupata muunganiko wa pamoja wa timu ili kuwa na kikosi imara.


Simba, juzi Jumatano
ilianza vizuri vita ya kuwania ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Selem View Academy, ambapo leo Ijumaa Simba wanatarajia kuvaana na Mlandege
majira ya saa 2:15 usiku
huku ikihitaji kushinda mchezo huu ili kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo.


Katika mchezo huo
wa juzi, Simba ilijaribu baadhi ya mastaa wapya ambao wapo kwenye majaribio ambao ni; Sharraf Shiboub na Muivory Coast, Mounkoro Tenena, ambao kuna uwezekano wakasajiliwa katika
kipindi cha dirisha hili
dogo la usajili.


Akizungumza na
Championi Ijumaa, kocha Pablo alisema: “Tupo kwenye kipindi cha usajili wa dirisha dogo, ni wazi kuwa matumaini ya kocha yoyote ni kuhakikisha anakuwa na kikosi bora, ndicho ambacho tunakifanya kwa sasa kwa kujaribu kuona ni nyota gani tunawasajili kwa ajili ya kuboresha kikosi chetu.


“Baada ya kukamilisha
mchakato wa kusajili wachezaji bora, kazi kubwa itakayobaki kwangu kama kocha ni kuhakikisha natengeneza muunganiko, ambapo tayari nimeandaa programu maalum ili kupata matokeo bora kutoka kwa kila mchezaji.”

Stori: Joel Thomas, Dar es Salaam

The post Pablo Aanza na Majembe Mapya Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz