Mtanzania Kutua Barcelona-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mtanzania Kutua Barcelona-Michezoni leo

NYOTA mwenye asili ya Tanzania, Akram Afif ametajwa kuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao kocha wa Barcelona, Xavier Hernandez amepanga kuwasajili mwishoni mwa msimu wakati wa kiangazi kwa ajili ya kukijenga upya kikosi chake.

 

Xavi anaamini kuwa Afif ambaye baba yake ni Mtanzania aliyewahi kuichezea Simba, anaweza kuongeza makali kwenye kikosi chake kama ilivyokuwa Qatar.

 

Kocha huyo wa sasa wa Barcelona, anamfahamu vizuri Afif kwani wawili hao waliwahi kufanya kazi pamoja tena yenye mafanikio makubwa kwenye klabu ya Al Sadd.

 

Ripoti kutoka Qatar zinasema kuwa Barcelona wanamfuatilia kwa karibu winga huyo wa kushoto mwenye miaka 25 na wapo tayari kuweka mezani Euro 2.70m (Sh7 bilioni).

 

Kama Barcelona watapata saini ya winga huyo basi hii itakuwa awamu ya pili kwa Afif kucheza Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’, awamu yake ya kwanza aliichezea Villarreal.

 

Winga huyo mwenye asili ya Tanzania amekuwa kwenye vichwa vya habari huko Qatar kwa kipindi kirefu kutokana na makubwa ambayo amekuwa akiyafanya.

The post Mtanzania Kutua Barcelona appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz