Morrison Akili Yote Fainali Mapinduzi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Morrison Akili Yote Fainali Mapinduzi-Michezoni leo

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mghana, Bernard Morrison, amefunguka kwamba, kwa sasa anajipanga kuhakikisha anaisaidia timu yake kushinda mechi ya nusu fainali na kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi.


Kauli ya Morrison
imekuja baada ya Simba kumaliza kinara wa Kundi C ikikusanya pointi nne katika michuano hiyo inayoendelea Zanzibar na kutinga nusu fainali ikitarajiwa kucheza na Namungo, kesho Jumatatu.


Katika mchezo wa mwisho
wa hatua ya makundi uliochezwa juzi Ijumaa kwenye Uwanja wa Amaan,
Simba ilishindwa kufungana
na Mlandege.


Akizungumza na
Spoti Xtra, Morrison amesema kuwa: “Mlandege ni timu nzuri, hii sio mechi yetu ya kwanza kukutana, huko nyuma tushawahi kucheza nao, ni timu yenye ushindani mkubwa sana.


“Tulijitahidi kuhakikisha
tunapata ushindi, lakini tumeukosa. Kwa sasa tunaangalia hatua inayofuata ya nusu fainali ambayo tutahakikisha tunashinda na kuingia fainali kwenda kuchukua ubingwa.”

STORI: CAREEN OSCAR, ZANZIBAR

The post Morrison Akili Yote Fainali Mapinduzi appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz