Mkataba wa Mshery Kufuru Tupu Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mkataba wa Mshery Kufuru Tupu Yanga-Michezoni leo

KATI ya wachezaji wapya wa Yanga waliosajiliwa katika dirisha dogo, basi mkataba wa kipa wa zamani wa Mtibwa Sugar, Abdoultwalib Mshery ndiyo kufuru hadi hivi sasa.

Mshery ni kati ya wachezaji wapya wazawa waliosajiliwa sambamba na kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wengine Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ na Denis Nkane akitokea Biashara United.

Yanga ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa baadhi ya wachezaji wa kigeni akiwemo Chico Ushindi ambaye ni mshambuliaji wa TP Mazembe ya DR Congo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, kipa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 50Mil baada ya kufikia muafaka mzuri na timu yake aliyokuwa anaichezea ya Mtibwa.

Mtoa taarifa huyo tofauti na dau hilo la usajili, mabosi wa Yanga wakaongeza kipengele katika mkataba wake ambao utainufaisha timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar aliyokuwa anaichezea.

Aliongeza kuna kipengele hicho cha Mtibwa kupatiwa asilimia tano pale kipa huyo kiwango kitakapokuwa kinaongezeka katika kila msimu kwa kipindi chote atakachokuwepo Yanga.

“Mkataba wa Mshery na Yanga una sharti la kuinufaisha timu yake ya zamani ya Mtibwa ambayo itakuwa inapata asilimia tano katika kila msimu pale kiwango chake kitakapoongezeka.

“Kipengele hicho cha mkataba wake amepewa Mshery pekee katika kuhakikisha anakuwa bora kila atakapocheza mchezo wa Ligi Kuu Bara au mashindano mengine.

“Yanga wenyewe ndiyo wameweka kipengele hicho katika kujenga mahusiano mazuri kati yao na Mtibwa,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Mkataba ni siri kati ya mchezaji na uongozi.”

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Mkataba wa Mshery Kufuru Tupu Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz