Mbeya City Wamfuata Kabwili-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mbeya City Wamfuata Kabwili-Michezoni leo

UKISEMA wa nini wenzako wanajiuliza watampata lini. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Mbeya City ambapo inaelezwa kuwa imepeleka ofa ya kumsajili kipa namba tatu wa Yanga, Ramadhan Kabwili.


Chanzo kutoka Yanga, kimeliambia Spoti
Xtra kuwa: “Wakati viongozi wakiwa katikamchakato wa kumuondoa Ramadhan Kabwili kikosini, kuna klabu ya ligi kuu imetuma barua ya kuhitaji huduma yake.


“Barua imeletwa Jangwani kutoka Klabu
ya Mbeya City ambayo imeonesha nia ya dhati kabisa ya kuhitaji huduma ya Kabwili.


“Viongozi tayari wamepata mbadala
wake ambapo jina la kipa wa Mtibwa Sugar, Abutwalib Mshery likiwa
limepitishwa na kinachofuata ni
mazungumzo kati ya klabu hizo mbili.”

 

Alipotafutwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli kuzungumzia hilo, alisema: “Masuala ya usajili yatakapokamilika yatawekwa wazi na klabu, lakini mpaka sasa tumeshamtangaza Salum Aboubakar.


“Tumewaacha wachezaji wawili
ambao ni Adeyum Saleh na Ditram Nchimbi, kama kutakuwa na wengine tutawatangaza.”

STORI: LEEN ESSAU, DAR

The post Mbeya City Wamfuata Kabwili appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz