Mayanga, Mayele Wana Vita Yao-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mayanga, Mayele Wana Vita Yao-Michezoni leo

UKIWEKA kando ile vita ya kusaka pointi tatu leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Arusha kati ya Polisi
Tanzania inayonolewa
na Malale Hamsini dhidi ya Yanga inayonolewa na Nasreddine Nabi, kuna bato ya ufungaji bora.


Bato hiyo ya kibabe
inatarajiwa kuwashuhudia washambuliaji wawili ambao ni namba moja kwenye timu zao ambapo ni Vitalis Mayanga kwa upande wa Polisi Tanzania na Fiston Mayele kwa upande wa Yanga.


Mayanga ametupia mabao
matano kibindoni kati ya11 na ametoa pasi tatu za mabao na kumfanya ahusike kwenye mabao nane, huku Mayele akiwa ametoa pasi moja ya bao na kufunga mabao sita na kumfanya ahusike kwenye mabao saba.


Ni mechi 11 kati ya 12
Mayanga ameanza kikosi cha kwanza ndani ya Polisi Tanzania, huku Mayele akiwa amecheza mechi zote 12.


Katika mchezo huo wa leo,
wawili hao wanatarajiwa kuziongoza timu zao kusaka ushindi kwani wana uhakika wa kuanza kila wanapokuwa fiti.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, DAR ES SALAAM

The post Mayanga, Mayele Wana Vita Yao appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz