Kocha Simba: Nilijua Nitawafunga Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kocha Simba: Nilijua Nitawafunga Yanga-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba Queens, Sebastian Nkoma, amefunguka kuwa kwa upande wake alikuwa anatambua ni lazima atawafunga wapinzani wake, Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu Wanawake lakini hakujua atawafunga kwa idadi gani ya mabao.

 

Katika mchezo huo uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar, Simba Queens iliibuka na ushindi wa mabao 4-1. Simba imeendeleza rekodi yake ya kuifunga Yanga kwenye ligi hiyo kuanzia msimu wa 2018-19.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Nkoma alisema kuwa: “Binafsi nawaheshimu wapinzani wangu kwa sababu kwa misimu miwili nimekuwa nawania nao ubingwa maana wao ni timu kubwa ambayo imekuwa na ushindani mzuri katika hii ligi.

 

“Lakini suala la kuwa leo (juzi) Simba itashinda hilo nilikuwa nalijua wazi japokuwa sikuwa najua kwamba tutashinda kwa idadi kubwa ya mabao ambayo tumeweza kushinda mbele yao.”

IBRAHIM MUSSA, DAR ES SALAAM

The post Kocha Simba: Nilijua Nitawafunga Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz