Familia Yamuondoa Mayele Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Familia Yamuondoa Mayele Yanga-Michezoni leo

  MSHAMBULIAJI tegemeo katika kikosi cha Yanga Mkongomani, Fiston Mayele jana asubuhi alirejea nyumbani kwao, DR Congo kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia.


Mshambuliaji huyo anaondoka nchini baada ya juzi
kutoka kuifungia timu yake bao la kuongoza katika
ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa
kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


Mkongomani huyo anatarajiwa kuukosa mchezo wa
kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa Jang’ombe kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


Yanga inatarajia kucheza mchezo
wake wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi hidi ya Taifa Jong’ombe
Januari 5, mwaka huu mchezo
utakaopigwa saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan mjini Unguja.


Chanzo cha habari kutoka ndani
ya uongozi wa Yanga, alipatwa na msiba wa shemeji yake Ijumaa iliyopita saa chache kabla ya mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji ambao ulimalizika kwa kushinda mabao 4-0.


Chanzo hicho kilisema kuwa mshambuliaji huyo
ruhusa ya kwenda kuhani msiba huo ambaye atarejea nchini Januari 7, mwaka huu na moja kwa moja ataungana na timu Zanzibar.


“Mayele alipanga kuondoka kwenda Congo kuhani
msiba wa shemeji yake leo (Jumapili) na ataungana na timu visiwani Zanzibar baadaye,” kilisema chanzo hicho.


Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo,
Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo alisema kuwa
“Ni kweli Mayele hayupo na timu amerejea nyumbani
kwao kwa ajili ya kwenda kuhani msiba wa shemeji yake lakini haraka atarejea baada ya kumaliza.”

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA, Dar

The post Familia Yamuondoa Mayele Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz