Fainali ya Kisasi Mapinduzi ni Azam vs Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Fainali ya Kisasi Mapinduzi ni Azam vs Simba-Michezoni leo

HII ni fainali ya kisasi ikiwa kutanisha Simba dhidi ya Azam, katika mchezo utakaopigwa kesho kutwa Alhamisi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


Ni fainali ya Kombe la
Mapinduzi kwa msimu wa 16. Azam imebeba ubingwa huo mara tano, huku Simba ikibeba mara tatu Timu hizi zinakwenda kukutana katika fainali ya nne kwenye michuano hii, baada ya mara tatu zote Azam FC kuibuka na ushindi Fainali ya kisasi mwaka 2012, 2017 na 2019 ambayo ilikuwa mara ya mwisho kwao kukutana.

azam

Jana Jumatatu, Azam FC ilikuwa ya kwanza kutinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Yanga kwa penalti 9-8, huku Simba ikija kuifunga Namungo mabao 2-0 yaliyofungwa na Meddie Kagere dakika ya 15 na Pape Sakho dakika ya 49.


Azam na Simba
zinakutana tena uwanjani baada ya kupita siku 13 tangu mara ya mwisho kupambana ndani ya Ligi Kuu Bara na Simba kushinda 2-1. Ilikuwa Januari Mosi, mwaka huu.

STORI: KAZIJA THABIT NA CAREEN OSCAR

The post Fainali ya Kisasi Mapinduzi ni Azam vs Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz