CAMEROON NA GAMBIA ZATINGA ROBO FAINALI AFCON-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

CAMEROON NA GAMBIA ZATINGA ROBO FAINALI AFCON-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

WENYEJI, Cameroon wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Comoro usiku wa Jumatatu Uwanja wa Paul Biya Jijini Yaoundé.
Mabao ya Cameroon yamefungwa na Karl Toko Ekambi dakika ya 29 na Vincent Aboubakar dakika ya 70, wakati la Comoro limefungwa na Youssouf M'Changama dakika ya 81.

Comoro ilipata pigo la mapema kufuatia kiungo wake, Jimmy Abdou kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya sita.
Comoro iliingia kwenye mchezo huo bila wachezaji wake nyota 12 wakiwemo makipa wote watatu kwa sababu ya majeruhi na kukutwa na virusi vya corona.


Lakini beki wa kushoto wa Ajaccio, Chaker Alhadhur aliyesimama langoni alifanya kazi nzuri mno.
Katika mchezo uliotangulia, Gambia iliitupa nje Guinea kwa kuichapa 1-0, bao pekee la mshambuliaji wa Bologna ya Italia, Musa Barrow dakika ya 71 Uwanja wa Bafoussam.
Sasa Cameroon itakutana na Gambia katika Robo Fainali Jijini Douala Jumamosi.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz