Bwalya: Tunazidi Kuingia Kwenye Mfumo wa Kocha-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Bwalya: Tunazidi Kuingia Kwenye Mfumo wa Kocha-Michezoni leo

RALLY Bwalya, kiungo wa Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco amesema kuwa bado wanaendelea kuingia kwenye mfumo wa kocha huyo ambaye anawasisitizia wapambane kupata matokeo.

Pablo alibeba mikoba ya Didier Gomes ambaye alibwaga manyanga kutokana na timu hiyo kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sasa ana kazi ya kupambania Kombe la Mapinduzi lililo mikononi mwa Yanga.

Bwalya mkononi ana tuzo ya mchezaji bora wa mchezo ambayo aliipata kwenye mchezo dhidi ya Selem View uliochezwa Uwanja wa Amaan wakati Simba ikishinda kwa mabao 2-0.

Nyota huyo alisema: “Kikubwa ambacho tunakifanya ni kuona kwamba tunapata matokeo na tunazidi kuona namna gani tunaweza kwenda na mfumo wa mwalimu ambaye anatufundisha na amekuwa akituambia kwamba tunapaswa kushinda mechi zetu ambazo tunacheza.”

Simba imetinga hatua fainali ya Kombe la Mapinduzi jana baada ya kuitungua Namungo FC kwa bao 2-0. Simba atakutana fainali ya AZAM FC ambaye alimfunga Yanga katika nusu fainali ya kwanza kwa mikwaju ya penati 9-8 baada ya kutoka sare dakika 90.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

The post Bwalya: Tunazidi Kuingia Kwenye Mfumo wa Kocha appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz