Ahmed: Yanga Wanatamani Kuwa na Mtu Kama Mimi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Ahmed: Yanga Wanatamani Kuwa na Mtu Kama Mimi-Michezoni leo

OFISI Menaja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema klabu ya Yanga wanatamani kuwa na mtu kama yeye ndio maana alipochukuliwa na Simba wakaanza kufukua mafaili yake ikiwemo picha alizopiga na Yanga.

 

Ahmed amesema hayo leo, Jumatano, Januari 19, 2022 wakati akifanya mahojiano na Kituo cha Radio cha WASAFI FM jijini Dar es Salaam.

 

“Yanga wanatamani kuwa na mtu kama mimi, ndiyo maana baada ya uteuzi wangu wakawa wanahaha kuanza kutafuta mafaili kuonyesha kwamba huyo pia ni Yanga, hii ni ishara kwamba hata wao wanatamani kuwa na mtu kama mimi.

 

“Angeteuliwa hafisa habari wa kawaida kawaida pale simba, wasingehangaika kufukua mafaili, wasinge hangaika kutafuta taarifa zangu, lakini kwa kuwa nimeteuliwa mimi ambaye wananipenda, wananihitaji niwe pale kwao ndio maana wakaanza kuhangaika,” amesema Ahmed Ally.

The post Ahmed: Yanga Wanatamani Kuwa na Mtu Kama Mimi appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz