Wazambia Kuwafanyia Undava Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Wazambia Kuwafanyia Undava Simba-Michezoni leo

UONGOZI wa timu ya Red Arrows ya Zambia, umeweka wazi wamepanga kulipa kisasi katika mchezo
wa marudiano dhidi ya Simba
licha ya kufungwa mabao mengi kutokana na mvua iliyoharibu hali ya uwanja na kukwamisha mipango yao.

 

Timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Anga la Zambia, imepoteza mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho kwa mabao 3-0 dhidi ya Simba kabla ya mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa Jumapili ya Desemba 5 huko
Zambia ambapo mshindi wa jumla
ataenda makundi Shirikisho.

Akizungumza na Championi Jumatano, meneja wa timu hiyo Rio Flowers, alisema: “Tunaamini sasa ni wakati wa kulipiza kisasi cha kuhakikisha tunawaondoa kwa kuwafunga mabao mengi ili kuzidi yale ambayo wao wametufunga huko.

 

Ukweli tunawaheshimu kwa sababu ni timu bora lakini kwa upande wetu tunachotaka kukifanya ni kuhakikisha tunapata ushindi mkubwa hapa kwetu.”

Stori: Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

KOCHA PABLO kwa UNYONGE Azungumza – “HATUJACHEZA Vizuri KABISA, MSINIPONGEZE”

The post Wazambia Kuwafanyia Undava Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz