Taifa Stars Yatua Mbeya Kufurahi na Mashabiki-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Taifa Stars Yatua Mbeya Kufurahi na Mashabiki-Michezoni leo

Meneja masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Denis Tairo (katikati) akiwa na baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars ikiwa ni muondelezo wa kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars’ ambapo wachezaji hao walikutana uso kwa uso na mashabiki wao wa mkoa wa Mbeya.

 

 

KAMPUNI ya Serengeti imewakutanisha uso kwa uso baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars na mashabiki katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini Mbeya ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars’

Mchezaji wa Taifa Stars Bakari Mwamunyeto, akijibu moja ya swali kutoka kwa mashabiki wa soka wakati wa tukio lililowakutanisha wachezaji wa timu hiyo ya taifa na washabiki wao lililofanyika jijini Mbeya chini ya kampeni ya Nje ya Dimba na Stars inayoendeshwa na bia ya Serengeti Lager.

 

 

Kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars ‘inalenga kuwapa nafasi mashabiki wa Taifa Stars kukutana na nyota wanaowapenda katika baa zao na pia watapata fursa ya kuwauliza maswali kuhusu maisha yao nje ya soka pamoja kupiga nao picha za ukumbusho. Kampeni hiyo ya nchi nzima itadumu kwa miezi mitatu.

 

Akiongea wakati wa hafla hiyo, meneja masoko wa kanda za juu kusini ni wa SBL, Denis Tairo alisema bia ya Serengeti lager ikiwa kama shabiki mkuu wa Taifa Stars inajivunia kuwaletea mashabiki wa Taifa Stars mkoani Mbeya nyota inaowapenda na kuwapa nafasi kuzungumza nao na hivyo kuwafahamu kwa undani zaidi.

 

“Shabiki mkuu na mdhamini wa timu yetu ya taifa, Taifa Stars Bia ya Serengeti Lager leo amewakutanisha mashabiki wa hapa Mbeya uso-kwa-uso na nyota ambao mara nyingi wamekuwa wakiwaona uwanjani. Hii ni fursa pekee ya mashabiki kujua maisha ya nyota wao nje ya uwanjani,” alisema

 

Denis alisema kampeni hiyo ya nchi nzima itahusisha wachezaji wa Taifa Stars ambapo watatembelea mikoa ya Mbeya, Mwanza na Arusha na kukutana na mashabiki wao kupitia matukio kama pati za mwisho wa mwezi ‘Nje ya Dimba na Stars’.

 

Kwenye matukio kama hayo mashabiki wataweza pia kujishindia zawadi mbalimbali na ofa za bei yao pendwa ya Serengeti lager.

 

“Wachezaji watakuwa kwenye baa mbalimbali na wakati wateja  wetu wa bia ya Serengeti Lager wakiendelea kuburudika na bia yao pendwa iliyotengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 na isyoongezwa sukari, watapata nafasi ya kuwauliza maswali, kupiga picha na kupata sahihi zao,” alisema.

 

Aliwataka mashabiki wa Stars kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya bia ya Serengeti Lager Pamoja na kusikiliza redio kwaajili ya kujua lini na wapi nyota wa taifa Stars watakuwa.

The post Taifa Stars Yatua Mbeya Kufurahi na Mashabiki appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz