Sure Boy Achota Mil 80 Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Sure Boy Achota Mil 80 Yanga-Michezoni leo

USAJILI mpya wa kiungo mshambuliaji wa Yanga anayetoka Azam FC, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ umeigharimu Yanga jumla ya Sh Mil 80 kwa ajili ya kusaini mkataba huo wa miaka miwili.

 

Sure Boy alisaini mkataba huo wa kujiunga na Yanga jumanne ya wiki hii huku akiwa ameomba kuvunja mkataba wake naAzam FC hivi karibuni baada ya kuruhusiwa kurudi klabuni hapo.


Nyota huyo ni miongoni
mwa wachezaji watatu waliosimamishwa naAzam FC pamoja naAggrey Morris na
MudathirYahya kutokana na
utovu wa nidhamu.


Chanzo chetu kutokaYanga
kimeliambia Championi Ijumaa kuwa: “Siku ya Jumanne Sure Boy alikuwa makao makuu ya Yanga akiwa na viongozi ambapo alisaini mkataba akiwa na wakili, Simon Patrick.


“Ni mkataba wa miaka miwili
huku dau alilochukua kwa ajili ya kusaini mkataba huo ni milioni 80 za Kitanzania na kwa sasa anasubiri tuAzam wamruhusu ili ajiunge rasmi naYanga.”

Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi yaYanga ambaye pia anahusika na usajili, DominicAlbinus, alisema: “Siwezi kuzungumzia masuala ya usajili sasa hivi mpaka mambo yote yatakapokamilika ambapo taarifa itatolewa na klabu.”


Championi Ijumaa
pia lilimtafuta Hery Mzozo, Meneja wa Sure Boy, ambaye simu yake haikuwa ikipatikana hadi
tunakwenda mitamboni.

STORI: LEEN ESSAU, Dar es Salaam

The post Sure Boy Achota Mil 80 Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz