Simba Yajipiga Kifua Kundi D-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Yajipiga Kifua Kundi D-Michezoni leo

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mulamu Nghambi amesema wamepanga kuhakikisha Simba inapata ushindi katika mechi mbili za mwanzo, kwani ndizo zitawaweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

“Siku zote mechi mbili za kwanza za makundi ndizo zinaamua kama unaenda robo fainali au hauendi. Hata msimu uliopita, mechi mbili za mwanzo ndizo zilichangia kutufanya tuongoze kundi.

 

“Kwa maana hiyo tukishinda nyumbani dhidi ya Asec na kisha ugenini dhidi ya Gendarmerie tutakuwa katika nafasi nzuri ukizingatia mechi mbili zitakazofuata zitakuwa dhidi ya Berkane nyumbani na ugenini,” amesema Nghambi.

 

Ni mara ya kwanza kwa Simba kukutana na RS Berkane na Gendarmerie, lakini imekutana na Asec Mimosas katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2003 ambapo Simba ilishinda bao 1-0 nyumbani na ugenini ikapoteza 4-3.

The post Simba Yajipiga Kifua Kundi D appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz