RONALDO APIGA MBILI, MAN U YAILAZA ARSENAL 3-2-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

RONALDO APIGA MBILI, MAN U YAILAZA ARSENAL 3-2-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya Manchester United yamefungwa na Wareno, Bruno Fernandes dakika ya 44 na Cristiano Ronaldo mawili dakika ya 52 akimalizia pasi ya Marcus Rashford na 70 kwa penalti baada ya Martin Odegaard kumuangusha Fred.
Mabao ya Arsenal yamefungwa na Emile Smith Rowe dakika ya 13 akimalizia pasi ya Mohamed Elneny na Martin Odegaard dakika ya 54 akimalizia pasi ya Gabriel Martinelli.
Kwa ushindi huo mbele ya kocha mpya wa mtarajiwa, Ralf Rangnick, Manchester United inafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya saba, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 23 katika nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 14.


Wakati huo huo, Michael Carrick aliyekuwa kaimu kocha wa Man United baada ya kufukuzwa Ole Gunnar Solskjaer naye aliachia ngazi rasmi baada ya ushindi huo tayari kumuachia jukumu Ralf Rangnic.
Carrick amekuwa na klabu hiyo tangu mwaka 2006 alipowasili kama mchezaji kutoka Tottenham Hotspuras na katika kipindi chake akisukuma kandanda ameichezea mechi 464 Manchester United na kushinda mataji matano ya Ligi Kuu ya England, moja la Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA pia.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz