KOCHA mpya, Mjerumani Ralf Rangnick ameanza vyema Manchester United baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mbrazil, Fred dakika ya 77 na kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 24 na kusogea nafasi ya sita, wakati Crystal Palace inabaki na pointi zake 16 nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 15.
No comments:
Post a Comment